Shirika la HIMSO lenye makao makuu jijini Mbeya, limetoa pikipiki tano (5) kwa mkoa wa Songwe kwa ajili ya kuratibu shughuli mbalimbali za CHF iliyoboreshwa mkoani humo. Pikipiki zitatumiwa na ofisi za CHF Iliyoboreshwa za halmashauri za mkoa huo ambazo ni Momba, Ileje, Songwe, Tunduma na Mbozi. Pikipiki hizo za aiana ya YAMAHA na Honda zina thamani ya jumla ya shilingi milioni thelathini na nne na laki moja (TZS 34,100,000/=).

Wakati akikabidhi pikipiki hizo kwa niaba ya shirika la HIMSO, Mwenyekiti wa Bodi ya HIMSO, Dr. Charles Hosea Mbwanji alimuomba na kumsisitiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Mh Dr Seif Shekalaghe kuwa, pikipiki hizo ziende kufanya kazi zilizokusudiwa za uratibu wa CHF iliyoboreshwa, ili kufikia malengo ya mkoa ya uandikishaji kaya kwa asilimia 30 (30%) ifikapo Juni 2021.

“Mheshimiwa, naomba nikusisitize, pikipiki hizi ziende kufanya kazi ile tuliyokusudia ya kuratibu CHF Iliyoboreshwa katika ofisi za CHF za Halmashauri. Hii ni muhimu sana hasa katika safari yetu ya kufikia wana Songwe na CHF Iliyoboreshwa. Kama tunavyofahamu, tuna malengo ya kufikisa asilimia 30 ya wana Songwe ifikapo Juni mwakani. Pikipiki hizi zikasaidie kwenye safari hiyo.” Dr Mbwanji.

Dr. Mbwanji pia alifafanua kwamba katika tukio hilo anakabidhi pikipiki nne kwa ajili ya Halmashauri za Momba, Ileje, Songwe na Tunduma wakati Mbozi walishakabidhiwa pikipiki mwishoni mwa mwaka 2019.

Akipokea pikipiki hizo kwa niaba ya mkoa wa Songwe, Mh. Dr. Shekhalage alilishukuru shirika la HIMSO kwa jihitada zake katika kusaidia kufanikisha malengo ya mkoa kweye huduma za afya hususani katika CHF iliyoboreshwa. Dr Shekalaghe pia alimuhakikishia Mwenyekiti wa Bodi ya HIMSO kuwa atahakikisha pikipiki hizo zinafanya kazi katika malengo yaliyokusudiwa.

“Napenda kukushukuru Dr Mbwanji na shirika la HIMSO kwa kuwa wadau katika masuala ya afya na hasa CHF Iliyoboreshwa kwa mkoa wetu wa Songwe. Nikuhakikishie pia, pikipiki hizi zitaenda kufanya kile kilichokusudiwa. Na kuhakikisha hili linatendeka, nawasihi viongozi wa halmashauri mniletee mipango kazi na malengo yenu ya CHF Iliyoboreshwa, kwani bila kupata hayo, sitakabidhi pikipiki hizi kwenu.” Dr Shekalaghe.

Baada ya makabidhiano haya, kilifanyika kikao kwa ajili ya kupanga mikakati ya kuandikisha wananchi wengi zaidi kwenye CHF Iliyoboreshwa. Kikao hicho kilihudhuriwa na Mratibu wa CHF Iliyoboreshwa – Taifa kutoka TAMISEMI, Dr. Boniface Marwa, Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Dr Shekalaghe, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dr Nyembea H, Waganga Wakuu wa Wilaya, Waratibu wa CHF Iliyoboreshwa wa Mkoa na Halmashauri, Wasimamizi wa CHF Iliyoboreshwa ngazi ya Tarafa na Wawakilishi wa Waandikishaji ngazi za vijiji.

HIMSO kama mdau na mshauri wa mkoa wa Songwe kwenye utekelezaji wa CHF Iliyoboreshwa walishiriki pia.

Pikipiki nne zilizotolewa na HIMSO kwa ajili ya waratibu wa wilaya za Momba, Ileje, Songwe na Tunduma
0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published.